
Thor na Captain America
Avenger ni muendelezo wa baadhi ya ya filamu za marvel universe. Filamu inaanza pale Loki (Tom hilddleston) anaporudi tena dunia na kuiba “the Tesseract” an alien source of pure energy, na kutishia kuteka dunia nzima kwa msaada wa jeshi lake la viumbe kutoka dunia nyingine liitwalo “the chitauri”.
Nick Fury (Samuel L. Jackson), kiongozi wa covert government outfit inayoitwa S.H.I.E.L.D anaunda team ya super heroes iitwayo The Avengers (Robert Downey Jr,Chris Hemsworth, Chris Evans, Mark Ruffalo, Scarlett johnsson, Jeremy Renner) kuzuia mipango ya Loki.
Badalaya kufocus sana kwenyemuhusika mmoja, mwandishi /director Joss Whedon ametengeneza The Avengers katika balance. Na kuhakikisha kila muhusika anapata at least action sequence moja,wahusika wote wanaonekana na kupata nafasi ya kuwa na sehemu zao kwenye filamu. Captain America anahangaika kuuelewa ulimwengu mpya aliojikuta, Thor anamaumivu ya kumpoteza kaka yake, Iron man anakiburi na hataki kukosolewa au Hulk na woga wa nguvu alizonazo.Hata black widow na Hawkeye ambao hawakupewa kipaumbele katika mionekano yao ya mwanzo wanapata nafasi ya kuonekana, hivyo tuna pata uelewa mzuri zaidi wa wahusika hawa kwa kutumia pia backstories.
Whedon anajulikana kwa kutengeneza wahusika wenye akili,upeo na kukua ki hisia, na filamu hii inaendeleza umaarufu huo.filamu hii pia ina furahisha kote kwenye dialogue na hata physical humor( ambapo Loki anapambana na Hulk). Japokuwa inaanza kama imepooza ila inakuja pamoja haraka pale mwandishi/director anapo fanikiwa kuelezea story na kuchanganya high-tension fight na action sequence.

Asante kwa posting hii, ilikuwa ni kusaidia kabisa na habari nyingi