Kampuni au biashsra ndogo inapoamua kuanzisha ukurasa wa facebook (Facebook page) wanatarajia watu watakuja na kujiunga (Like) na ukurasa wao. Lakini mara nyingi haiko hivo. Ni pale njia mbali mbali zinapotumika kuhamasisha watu kujiunga(Like) ndipo ukurasa wa kampuni unaweza kupata watu. Kuna njia nyingi za kutumia kati ya hizo kuna nzuri na ambazo sio nzuri. Katika hi makala tutaongelea moja ya njia ambayo wengi huitumia lakini sio njia nzuri na pia tutakuonyesha njia kumi (10) nzuri unazoweza kutumia kuongeza wafuasi katika ukurasa wako.
NJIA ISIYOFAA
Mara nyingi njia ya kwanza ambnayo watu wengi wanatumia ili kuongeza watu wa kujiunga na ukurasa wao ni kualika marafiki zao WOTE kwa kutumia kitufe (Button) cha suggest to friends. Njia hii kwa wakati mwingine inaweza isikupe matokeo unayoyatajia. Utafiti uliofanyika na kwa watumiaji wengi wa facebook ni kwamba mtu hukerwa (Uudhika) anapopoke maombi ya kujiunga na ukurasa ambayo alishakataa maombi yake mara ya kwanza.
Kuna sababu kadhaa zinazosazoifanya njia kutokua nzuri sana kuhamasishia watu kuLIKE ukurasa wako
- Watumiaji wa facebook wanaruhusiwa kujiunga na kurasa 500 pekee, hii inawasababisha watu wengi kua makini katika kuchagua kurasa za kujiunga (Like). (Ingawa kuna uwezekano wa kuvuka kurasa 500)
- Maombi ya kujiunga na ukurasa yanaweza kuwa mengi kwa mtu mmoja. Kutokana na kwamba watu wengi wanatumia njia hii ya kualika marafiki kuLIKE ukurasa wao, hi inaweza kusababisha watu wengi kutuma kwa mtu mmoja hivo kuasabisha msongamano wa maombi
Habari njema kwako ni kwamba kuna njia ambazo unaweza kuzitumia na zikakupa matokeo;
#1 Weka ukurasa kwenye Email signature block
Ukitaka kupromoti ukarasa wako tumia email yako na ongeza LINK kwenye upande wa email signature, kila unaemtumia email ataona link inayompeleka kwenye ukurasa wako wa facebook na kama ni mteja itakua ni vizuri zaidi kwasababu atakua amepata njia nyingine ya kukufikia kirahisi na wewe utakua umepata shabiki (fan) wa ukurasa wako.
#2 Tengeneza kipande cha video kinachovutia cha ukaribisho
Tengeneza video fupi inayovutia inayoelezea a) Maudhui ya ukurasa wako b) Inalenga watu gani c) Kwa nini mtu ajiunge. Hi itakusaidia kuovutiwa na ukurasa wako kwasababu wanjua watakachokipata kutoka kwako.
#3 Tumia facebook Apps
Facebook Apps zinafanya watu kushiriki kwenye ukurasa wako kutokana na kwamba kuna Apps nyingi zinazochangamsha watu kwa mfano Kuna App ya kurushia video inayoitwa vpype. Hi inakuweza kurusha video moja kwa moja (Live streaming) na hivo unaweza kualika marafiki zako kutumia ukurasa wako binafsi na wakaja kuangalia unachorusha hii inaweza kukuongeza matangazo zaidi kwa sababu marafiki zako pia wanaweza kuwambia marafiki zao wengine.
#4 Wahamasishe mashabiki wa ukurasa wako waTAG picha zao
Kama huwa unaandaa matamashaau matukio ya kijamii piga picha kwenye matukio hayo na wahasishe mashabiki wa ukurasa wako waTag picha zao wenyewe. Hi itakuongezea matangazo ya bure kwenye Wall za mashabiki wako na pia marafiki zao kupitia news feed, hi ni kwa sababu picha zinaongea zaidi kuliko maneno.
#5 Weka matangazo ya facebook (Facebook Ad)
Hata kwa kutumia budget ndogo ndogo za wiki au mwezi unaweza kutumia njia hii ambayo inafanywa na facebook wenyewe. Matangazo ya facebook yamewezesha kurasa nyingi za facebook na websites kupata watu wengi wanaotembelea na baadhi yao hujiunga na kurasa hizo. Ili kununua matangazo ya facebook nenda kwenye sehemu ya chini kabisa ya ukurasa wako na bonyeza kwenye link iliyoandikwa “ Create an Ad” humo unaweza kujua ni kiasi gan cha watumiaji wa facebook wako katika soko unalolilenga.
Kwa kutangaza ukurasa wako na facebook kitufe cha like kinataonekana kwenye tangazo kama inavoneka kwenye picha hapo chini hivo watu wanaweza kuLIKE ukurasa wako hapo hapo kwenye tangazo na pia huonyesha baadhi ya marafiki ambao wamesha like huo ukurasa, hi pia uvutia marafiki wengine kuLIKE ukurasa.
#6 Unganisha (Link) ukurasa wako wa facebook na wa twitter
Kama una ukurasa wa twitter unaganisha (Link) na ukurasa wako wa facebook. Kama huna ukurasa wa twitter wahi kafungue haraka kwa sababu kujitangaza kwa njia ya mitandao ya kijamii (Social media marketing) itakupa matokeo mazuri pale utakapotumia mitandao mbalimbali (twitter, LinkedIn, google plus n.k)
Kwenye facebook unaweza kuandika herufi 420 wakati kwenye twitter mtu anarusiwa kuandika herufi 140 pekee. Hi inafanya unapoandika maneno zaidi ya 140 inaweka link inayomrejesha msomaji kwenye ukurasa wako wa facebook.
Pia unaweza kuutangaza ukurasa wako kwenye background ya ukurasa wako wa twitter, kwenye URL link pia kwenye twitter bio, LinkedIn bio, google plus bio na mitandao mingine ya kijamii unayojiunga nayo.
#7 Tumia machapisho (Print media)
Hakikisha machapisho yote unayoyatumia katika biashara yako yanawekewa ukurasa wako wa facebook (Na mitandao ya kijamii mingine ambayo unashiriki kama twitter na mingine). Weka link ya ukurasa wako wa facebook kwenye Business card zako, vipeperushi, majarida ya kampuni, matangazo ya kwenye magazeti, kwenye bidhaa n.k
#8 Weka tangazo kwenye sehemu yako ya biashara
Kama biashara yako ina office maalumu kwa mfano duka, super market, mgahawa, hoteli n.k weka kitangazo kidogo sehemu ya mbele au sehemu ya mapokezi ili kuwajulisha wateja wako kua unapatikana kwenye facebook. Wahamasishe wateja wako wajiunge kwa kutumia simu zao, unaweza kutoa motisha kwa kuweka zawadi kwa wateja watakaojiunga hapo hapo. Kwa mgahawa au hoteli unaweza kuonesha ukurasa wenu wa facebook kwenye MENU za chakula pia.
#9 Tumia @Tag
Kama na wewe umejiunga (Like) na ukurasa wako utakua na uwezo wa kuTag ( @Tag) ukurasa wako wa biashara kwenye ukurasa binafsi. Mara kwa mara unaweza kuwajulisha marafiki zako kinachoendelea kwenye ukurasa wako kwa kuandika ujumbe wako binafsi na kuTag ukurasa wako kwa kutumia @Tag. Ni rahisi kufanya hivi, we anza tu kuandika alama ya “@” ikifatiwa na herufi chache za jina la ukurasa wako, na itatokea menu yenye majina na ukurasa wako ukiwemo. Chagua ukurasa wako na utajiandika hap, lisipotokea kwenye menu endelea kuongezea herufi za jina.
#10 Tumia jina la ukurasa wako kama sahihi au utambulisho wako
Pale unapokua unaandika kwenye kurasa bi nafsi za marafiki zako au kwenye kurasa za mashabiki (Fan page) zingine tumia jina la ukurasa wako “@tag”(@jina la ukurasa) kama njia ya kumalizia au kuhitimisha ujumbe wako. Hi itasaidia ukurasa wako kuoneka maeneo mengi na watu wengi.
Mwisho: Sio kwamba njia ya “suggest to friends” haifai kabisa, hapana. Hi njia inaweza kutumika kwa mafanikio kutegemea kiasi cha marafiki ulionao, uhusiano ulionao na marafiki zako, Kiasi ambacho huwa utatuma maombi ya kujiunga na kurasa kwa marafiki zako.
